2 Samuel 7:13-18

13

aYeye ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya Jina langu, nami nitaimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.

14

bNitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu. Atakapokosea nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu, kwa adhabu ya kupigwa na wanadamu.

15

cLakini upendo wangu kamwe hautaondolewa kwake, kama nilivyouondoa kwa Sauli, niliyemwondoa atoke mbele yako.

16

Nyumba yako na ufalme wako utadumu milele mbele zangu, kiti chako cha enzi kitafanywa imara milele.’ ”

17Nathani akamwarifu Daudi maneno yote ya maono haya.

Maombi Ya Daudi

(1 Nyakati 17:16-27)

18 dNdipo Mfalme Daudi akaingia ndani, akaketi mbele za Bwana, akasema:

“Ee Bwana Mwenyezi, mimi ni nani, na jamaa yangu ni nini, hata umenileta mpaka hapa nilipo?

Copyright information for SwhKC